Monday, February 27, 2012

WAKAGUZI WA NDANI NDIO WASIMAMIZI WA RASILIMALI ZA NCHI KWA NIABA YA WANANCHI-MTONGA.

Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Mohamed Mtonga akifungua mkutano wa siku tatu wa wakaguzi wa ndani wa Halmashauri za Serikali za Mitaa na Sekretarieti za mikoa jijini Dar es salaam . Mkutano huo uliwajumuisha wakaguzi 165 kutoka mikoa yote ya Tanzania bara kwa lengo la kuwaelimisha juu ya miongozo ya ukaguzi wa ndani imetolewa hivi karibuni ili kuboresha ukuguzi wa ndani utakaoleta matokeo mazuri ya rasilimali na fedha za wananchi 
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa wakaguzi wa ndani wa Halmashauri za Serikali za Mitaa na Sekretarieti za mikoa wakisikiliza kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa jijini Dar es salaam kwenye mkutano wa  kuwaelimisha juu ya miongozo ya ukaguzi wa ndani imetolewa hivi karibuni ili kuboresha ukuguzi wa ndani utakaoleta matokeo mazuri ya rasilimali na fedha za wananchi.(Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO- Dar es salaam).
Na.Tiganya Vincent-MAELEZO- Dar es salaam
Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Mohamed Mtonga ameagiza wakaguzi wote wa ndani kuhakikisha kuwa wanasimamia rasilimali za nchi vizuri kwa niaba ya wananchi ili miradi ilinganishe na thamani ya  fedha  iliyoombewa.
Mtonga alitoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano wa siku tatu wa wakaguzi wa ndani wa Halmashauri za Serikali za Mitaa na Sekretarieti za mikoa jana jijini Dar es salaam .
Alisema inasikitisha kuona ubadhirifu wa mali za Serikali kama vile ujenzi wa madarasa hayakidhi viwango unatokea mita chache toka Ofisi kwa Mkaguzi wa Ndani  au mtaa anaoishi bila kuchukua hatua zinazostahili za kuhakiki kama kweli mradi huo unalingana na fedha zilizotolewa na Serikali.
Mtonga aliwaagiza wakaguzi wa ndani kuwa wabunifu ili wawe wasimamizi wazuri wa rasilimali na fedha umma kwa niaba ya wananchi bila kujali kuwa wanavifaa vya kutosha au hawana .
Aidha Mkaguzi Mkuu huyo wa Ndani wa Serikali aliwaonya Wakaguz hao kuepuka tabia ya Ushirikiano na mitandao inayowafanya kikiuka sheria na taratibu za fedha ambazo ndio zinaweza kusababisha kutoa taarifa zisizokuwa za sahihi za ukaguzi wa ndani na hivyo kusababisha upotevu wa fedha za umma.
Alisema kuwa inasikitisha kuona kuwa inatokea tukio kama la Halmashauri ya  Wilaya ya Kishapu ambalo lilitokana na ukaguzi maalumu wa mwaka 2007/2008 hadi 2009/2010 wakati Mkaguzi wa Ndani yupo .
Katika hatua nyingine Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Mtonga alisema kuwa Ofisi yake inaandaa Mwongozo utakaowasaidia wakaguzi wa Ndani kukaguzi bajeti na kuangalia utekelezaji wake.
Hatua hiyo inalenga kuhakikisha kunakuwepo kwa uwazi na uwajibikaji kwa watendaji ili mwananchi ajue bajeti inakwendaji na kitu gani kinatakiwa kufanyika ili kumletea maendeleo kulingana na mapendekezo ya vipaumbele vilivyoombewa fedha.

No comments:

Post a Comment