Monday, February 27, 2012

SPIKA MAKINDA AONGOZA MAELFU YA WATU KATIKA MAZISHI YA ALIYEKUWA DAP WA BUNGE.

Viongozi wa dini wakijiandaa kwa ibada ya kumuaga aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Utawala na rasilimali Watu na Mshauri Mkuu wa mambo ya Utawala  wa Ofisi ya Bunge la Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania  marehemu Leo Theodore Mnyanga aliyefariki dunia tarehe 22 Feb. 2012 na kuzikwa katika makaburi ya Mlima Kola nje kidogo ya mji wa Morogoro tarehe 26 Feb.  2012.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwaongoza waombolezaji  kwa kutoa salamu za rambirambi katika mazishi hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Ndugu Joel Bendera (kushoto), Spika Makinda na Mhe. Bura (kulia) wakimfariji mke wa marehemu (katikati).
Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa Ngugu Jossey Mwakasyuka akimwakilisha Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah katika kutoa salamu za rambirambi kwa niaba ya wafanyakazi wote wa ofisi ya Bunge.
Familia ya marehemu ikitoa heshima za mwisho kwa baba yao mpendwa.
Wafanyakazi wa ofisi ya Bunge wakiwa wamelibeba jeneza lenye mwili wa marehemu Mnyanya kuelekea makaburini.
Spika Makinda akiweka udongo kaburini.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Ndg. Joel Bendera akiweka shada la maua juu ya kaburi.

Watoto wa marehemu (Fred na kaka yake) wakitoa neon la shukrani kwa waombolezaji.(Picha zote na Prosper Minja -Bunge).

No comments:

Post a Comment