Kikosi kazi cha Twasa FC.
Na. Mwandishi wetu
Timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC Jumamosi itacheza mchezo maalum wa kirafiki na timu ya Friends of Simba kwenye uwanja wa TTCL Kijitonyama.
Mchezo huo umepangwa kuanza saa 2.00 asubuhi na maandalizi yake yamekamilika kwa mujibu wa mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary.
Majuto alisema kuwa sababu kubwa ya kuandaa mechi hiyo ni kuwakutanisha wadau wa michezo na waandishi wa habari na kubadilishana mawazo.
Alisema kuwa wachezaji wake wamejiandaa ili kuendeleza wimbi la ushindi kwa timu yake kwani tokea kuanza kwa mwaka huu, hawajapoteza hata mechi moja.
“ Tunatarajia kuwa na mechi ya kusisimua, nzuri na ngumu, hii inatokana na ukweli kuwa kila timu imejipanga na imedhamilia kuonyesha mchezo mzuri, tunaowaomba mashabiki kufika kushuhudia nurudani hiyo ya kina,” alisema Majuto.
Alisema kuwa wachezaji kadhaa wa Friends of Simba wameonyesha kupania mechi hiyo chini ya Mzee Hiza, Juma Ndambile (nahodha), Mlamu Ng’ambi, Patrick Ruta, Rodney Chiduo, Malolana na wengine wengi.
Majuto alisema kuwa Taswa FC imejipanga sana na wachezaji wake nyota watakuwepo. Baadhi ya wachezaji hao ni Saleh Ally, Super Deo, Ali Mkongwe, Faustine Felician, Wilbert Molandi, Sweetbert Lukonge na Juma Ramadhan.
Wengine ni Salum Jaba, Ibrahim “Maestro” Masoud, Mbozi Katala, Mohamed Mharizo, Saidi Seif, Martin, Monishiwa Lihambiko, Julius Kihampa, Mohamed Akida, Fred Ndembela, Fred Mweta, Elius Kambili, Hatim Naheka, na wengine wengi.
No comments:
Post a Comment