Monday, February 13, 2012

MJUMBE KAMATI YA UTENDAJI TFF AFARIKI DUNIA

Shirikishla Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiktaarifa za kifcha aliyewahi kuwa mjumbe wake wa Kamati ya Utendaji, Kassim Kashulwe kilichotokea Februari 9 mwaka huu nyumbani kwake Kigurunyembe mkoani Morogoro.

Licha ya kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF (wakati huChama cha Mpira wa Miguu Tanzania- FAT), pia Kashulwe aliwahi kuwa kiongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogor(MRFA) na baadaye kamishna wa mechi za Ligi Kuu. 

Kwa mujibu wa taarifa tulizopata le(Februari 13 mwaka huu) kutoka MRFA, Kashulwe alifia nyumbani kwake na kuzikwa juzi (Februari 11 mwaka huu) kwenye makaburi ya Kora yaliyoknje kidogya mji wa Morogoro.

Mbali ya Kashulwe, wengine waliochaguliwa katika uchaguzi wa FAT uliofanyika mwaka 1993 mjini Kibaha ni Muhidin Ndolanga (Mwenyekiti), Alhaji Omari Juma (Makamu Mwenyekiti) na Kanali Ali Hassan Mwanakatwe (Katibu Mkuu) na wajumbe Abdul Msimbazi, Amin Bakhresa, Job Asunga, Joel Bendera, Masalu Ngofilna Wilson Mwanja.

Msiba huni pigkwa familia ya Kashulwe, TFF na familia ya mpira wa miguu nchini kwa kuwa mchangwake ulikuwa badunahitajika. TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Kashulwe, na MRFA na kuwataka kuwa na uvumilivu kipindi hiki cha msiba humzito.
Pia TFF itatoa ubani wa sh. 200,000 kwa familia ya marehemu kama rambirambi zake. Mungu aiweke rohya marehemu Kashulwe mahali pema peponi. Amina
 
Boniface Wambura, Ofisa Habari
Shirikishla Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

CHANZO ..LUKAZA BLOGSPOT.

No comments:

Post a Comment