Thursday, February 23, 2012

BALOZI WA IRAN NA RAIS WA KITUO CHA UTAMADUNI NA UHUSIANO WA KIISLAM CHA NCHINI IRAN WAMTEMBELEA WAZIRI WA HABARI, WAAHIDI USHIRIKIANO NA TANZANIA.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanueli Nchimbi (kulia) akizungumza na Rais wa Kituo cha Utamaduni na Uhusiano wa Kiislam kutoka nchini Iran Dkt. Mohammed Basheir Khurrqmshad (kushoto)  mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara hiyo leo jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine Rais huyo ameahidi kuendeleza ushirikiano kati ya Tanzania na Iran katika sekta ya utamaduni na michezo ikiwemo kusaidia kuleta makocha wa mchezo wa riadha.
Balozi wa Irani nchini Tanzania (katikati) Movahedi Ghomi akimweleza jambo waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt. Emmanueli Nchimbi (kushoto) mara baada ya kumtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Rais wa Kituo cha Utamaduni na Uhusiano wa Kiislam cha  Iran Dkt. Mohammed Basheir Khurrqmshad.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Emmanueli Nchimbi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali ya Iran waliomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es salaam.(Picha na Aron Msigwa –MAELEZO).

No comments:

Post a Comment