Friday, August 3, 2012

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Asiye na Wizara Maalumu, Profesa Mark Mwandosya Arejea Bungeni



 WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Asiye na Wizara Maalumu, Profesa Mark Mwandosya (juu),jana alikuwa kivutio kikubwa bungeni na kuwafanya wabunge wamshangilie kwa muda mrefu wakati akitambulishwa.

Mwandosya ambaye alikuwa Waziri wa Maji kabla ya mabadiliko yaliyofanyika miezi mitatu iliyopita alishindwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa muda wa mwaka mmoja, kwa sababu ya matatizo ya kiafya. 

Waziri Mwandosya aliingia bungeni jana asubuhi muda mfupi baada ya kumalizika kwa maswali na majibu, hivyo kuwafanya wabunge kulipuka kwa makofi na vigelegele.

No comments:

Post a Comment