Friday, August 3, 2012

MWALIKO KWA WATANZANIA WAISHIO LONDON NCHINI UINGEREZA KUJUMUHIKA NA WENZAO WA AFRIKA YA MASHARIKI KATIKA HAFLA FUPI YA UFUNGUZI WA SHUGHULI ZA BENKI YA KCB HAPA NCHINI UINGEREZA





Mheshimiwa Balozi, akiwa kwenye picha ya pamoja na Wawakilishi wa Benki ya KCB Tanzania LTD. Pili (Kulia), Balozi Peter Kallaghe, (kwanza kulia) Dada Shose Kombe, Bwana James Agin, Dada Pamela Baguma na Naibu Balozi, Mh. Chabaka Kilumanga.
***********
UBALOZI WA TANZANIA, LONDON, KWA NIABA YA BENKI YA KCB TANZANIA LIMITED INAWAALIKA WATANZANIA WOTE WAISHIO UINGEREZA, KUJUMUHIKA NA WENZAO WA AFRIKA YA MASHARIKI KATIKA HAFLA FUPI YA UFUNGUZI RASMI WA SHUGHULI ZA BENKI YA KCB NCHINI UINGEREZA, KWA WAISHIO UGHAIBUNI (DIASPORA).


HAFLA HIYO FUPI YA UFUNGUZI AMBAYO ITAWAJUMUISHA WAAFRIKA MASHARIKI, INA LENGO LA KUPANUA WIGO WA SHUGHULI ZA BENKI YA KCB HAPA UINGEREZA, KUTANGAZA SHUGHULI ZA UTENDAJI WAKE KATIKA KUWASAIDIA WANANCHI WA JUMUHIYA YA AFRIKA YA MASHARIKI KATIKA KUWEKEZA KIBENKI, KUFUNGUA AKAUNTI ZA AINA TOFAUTI, KUJIWEKEA AKIBA, KUWEKEZA NYUMBANI (TANZANIA), NJIA MBALIMBALI ZA KUTUMA NA KUPOTEKEA PESA KWA NJIA YA MTANDAO (INTERNET), KUTUMA PESA KWA KUTUMIA SIMU ZA MKONONI (MOBILE PHONES), IPADS NA NYINGINEZO.


HALFA HIYO , ITAFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI 4 AUGUST 2012, KUANZIA SAA 16:00pm, KWENYE HOTEL YA HOLIDAY INN, BLOOMSBURY, CORAM STREET, LONDON, WC1N 1HT.

No comments:

Post a Comment