Neema Kumba (kushoto) akipokea fomu ya kuwania nyadhifa hizo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Oganizesheni na siasa UVCCM, Taifa, Sophia Duma, .
***
KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia umoja wa vijana wa (UVCCM) na Msomi wa digrii ya uchumi, Neema Kumba amejitosa kwenye uchaguzi mkuu wa umoja huo Taifa kwa kuchukua kugombea nafasi ya NEC na uwakilishi UWT.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Ijumaa Agosti 3 jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kukabidhiwa fomu hiyo na Mkuu wa Idara ya Oganizesheni na siasa UVCCM, Taifa, Sophia Duma,
Kumba ambae awali alikua Katibu wa CCM, tawi la North London, Nchini Uingereza,alipokua akichukulia digrii yake ya uchumi, alisema lengo ni kuakikisha mikakati thabiti inajengeka kwa kiwango kikubwa miongoni mwa vjana na wanawake wote nchini.
“Kwa umakini wangu na maarifa niliyoyapata kwenye elimu na uwepo wangu ndani ya chama, ndani na nje ya nchi, ni wakati sasa na mimi kuwasaidia wenzangu hasa Vijana na wanawake ambao mara nyingi wamekua wakisahauriwa na huu ndio wakati wa kuwainua” alisema Kumba.
Mbali na kuchukua fomu hiyo ya NEC na uwakilishi UWT, Taifa, pia tayari alisha chukua fomu ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti Uvccm, Wilaya Ilala.
Mpaka sasa tayari wanachama mbalimbali wa UVCCM, wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania uongozi ambapo mwisho wa kurudisha fomu hizo, Agosti 6.
No comments:
Post a Comment