Wednesday, July 4, 2012

UREKEBISHAJI MPAKA PORI LA AKIBA SELOUS WAKUBALIWA NA KAMATI YA URITHI WA DUNIA.

Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Tanzania Balozi Khamis Kagasheki akisisitiza kuwa ombi lililopelekwa katika kamati ya urithi wa dunia ya UNESCO mwezi Januari 2011, lilijadiliwa katika kikao chake cha 35 ambacho kilihamishia mjadala huo katika kikao cha 36 kinachoendelea.
Na.MO BLOG TEAM
Kamati ya Urithi wa Dunia ya UNESCO katika kikao chake cha 36 kinachoendelea katika jiji la Saint Petersburg nchini Russia imekubali ombi la Tanzania la kuurekebisha mpaka wa Pori la Akiba la Selous, ambalo ni eneo la urithi wa dunia, ili kuruhusu uchimbaji wa madini ya Urani.
Eneo hilo linalohusika ni asilimia 0.8 ya eneo la Pori la Akiba la Selous.
Uamuzi huo ulifanyika ili kuruhusu Tathmini ya Athari ya Mazingira (EIA) kukamilishwa na kutoa muda kwa wataalam wa IUCN kufika eneo linalohusika ili kuliona na kuhakiki taarifa ya tathmini hiyo.
Akizungumzia suala hilo Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Balozi Khamisi Kagasheki amesema uamuzi uliotolewa na Kamati ya Urithi ya Dunia itaipa Tanzania uwezo na fursa nzuri ya kutimiza malengo ya kiuchumi.


No comments:

Post a Comment