Wednesday, July 4, 2012

KITANDADUARA CHAVUTIA WENGI KATIKA BANDA LA VETA KWENYE MAONESHO YA SABASABA.






Baadhi ya wateja wakionekana kuingia na kutoka katika banda la VETA wakati wa maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Wateja wakishangaa ‘Kitanda Duara’ katika banda laVETA katika maonyesho hayo. Hichi ni kitanda cha kisasa kinaweza kuwekwa katika muonekano tofauti na kufanya kila anayekutembelea nyumbani au hoteli kuvutiwa nacho. Anayetoa melekezo (kulia) ni Mwanafunzi Fani ya Useremala VETA Shinyanga Msengiyumva Stephano Kalabwe.
Meneja Uhusiano wa Umma wa VETA Geace Patricia Kabogo akionyesha moja bidhaa wanazotengenza ambayo ni ‘Kabati ya Vifaa Vya Siri Ofisini’ wakati wa maonyesho ya kibiashaya ya kimataifa ya sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Kabati hilo hutumika ofisini au sehemu ya kazi mbalimbali, hasa kwa kutunza nyaraka nyingi au zote za muhimu za siri katika ofisi
 Mwanafunzi wa VETA Mikumi Yunus John akitonyesha ubunifu wa mfumo bora wa umeme wa magari katika maonyesho ya Sabasaba.
Mwalimu Mwachambi wa Chuo cha VETA Dodoma akitoa maelekezo juu ya jinsi ‘Josho la Kisasa’ linavyoweza kutumika kuoshea mifugo ambalo pia linahamishika kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Mwanafunzi VETA Kigamboni Salum Machapati(wa pili kulia) akitoa maelezo kuhusu ‘Kitanda Tiba’  ambacho ni cha kisasa na hutumika katika sehemu ya hali ya hewa yoyote na kimeundwa kwa mbao, udongo pamoja na mkaa. VETA wanasema ni vizuri kulala na kukaa zaidi katika kitanda hicho kwa vile juu ya kitanda huwekwa ‘tiles’ za udongo pamoja na godoro jembamba sana kwa makusudi ya kunyoosha mgongo wakati wa kulala.

No comments:

Post a Comment