Tuesday, July 3, 2012

BALOZI IDD AWATAKA MABALOZI WA HESHIMA KUZITANGAZA TANZANIA NA ZANZIBAR KWA WAWEKEZAJI WA NJE.



Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Mabalozi wa Heshima wa Tanzania katika baadhi ya Majimbo ya Marekani Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Kulia kwa Balozi idd ni Balozi wa Tanzania Washington D.C Bibi Mwanaidi Sinare, Bw. Kjell Berg wa Minessota na Bw.  Ahmed Issa Alqassim wa San Francisco. 
Kushoto kwa Balozi ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Khalid Slum Moh’d, Naibu wake Nd. Said Shaaban pamoja na Bw. Saleh ambae ni Msaidizi wa Balozi Jimbo la Washington

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa zawadi kwa mmoja wa Wafanyabiashara Waandamizi waliounda Kundi la VIP Safari kutoka Nchini Marekani ambao wapo Nchini kuangalia uwezekano wa namna ya Kampuni zao kuwekeza Vitega Uchumi Nchini Tanzania.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Wafanyabiashara Waandamizi wa Kundi la VIP Safari baada ya kuwaandalia chakula cha usiku kwa balozi Serena Inn Hoteli Shangani Mjini Zanzibar.
Kulia ya Balozi Seif ni Balozi wa Tanzania Washington D.C Bibi Mwanaidi Sinare na Balozi wa Heshima MjiniMinessota Bw. Kjell Berg.
Kushoto kwa balozi ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk, Mke wa Balozi Seif Mama Asha Suleimana Iddi pamoja na Mmoja wa Wafanyabiashara wa VIP Safari. (Picha na  Saleh Masoud wa OMPR-ZNZ).
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Mazingira ya Kimaumbile yaliyoizunguka Zanzibar bado yana fursa nzuri ya kutumiwa katika shughuli za Uwekezaji Vitega Uchumi.
Katika mazungumzo yake na mabalozi wawili wa Heshima wa Tanzania katika majimbo mawili ya Marekani ya Minessota na San Francisco Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar, Balozi Seif amesema katika kuyatumia vyema mazingira hayo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inajaribu kuongeza nguvu za uimarishaji wa miundo mbinu katika Sekta ya Utalii.
Mabalozi hao Bw. Ahmed Issa Qassim atakayeiwakilisha Tanzania katika Jimbo la San Francisco na Bw. Kjell Berg wa Jimbo la Minessota waliongozwa na Balozi wa Tanzania Mjini Washington D.C Balozi  Mwanaidi Sinare Maajar.
Amesema licha ya Sekta ya kilimo kuchukuwa nafasi kubwa ya Uchumi wa Taifa lakini eneo la utalii pia lina fursa nzuri ya kuwa muhimili wa Pili wa Uchumi wa Zanzibar kwa hivi sasa.
Balozi Seif amefahamisha kwamba serikali inaangalia pia uwekezaji wa maeneo ya Kumbi za Mikutano ya Kiutalii kutokana na kupanuka zaidi kwa sekta hiyo hivi sasa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif amewaomba Mabalozi hao wa Heshima wa Tanzania katika Majimbo ya Marekani kuwa wawakilishi wazuri wa kuitangaza Tanzania na Zanzibar kwa ujumla kwa wawekezaji kwenye majimbo watakayoyafanyia kazi.
Balozi Serif amewaahidi wawakilishi hao kwamba Serikali zote mbili zitajitahidi kutoa msaada kwao kwa vile kazi watakazokwenda kuzifanya ni kwa ajili ya Watanzania.
Mapema Balozi wa Tanzania Mjini Washington D.C Bibi Mwanaidi Sinare Maajar alisema Zanzibar bado ina Utajiri wa Kihistoria ambao Wamarekani walio wengi wanaendelea kuushangaa.
Balozi Mwanaidi amesema utafiti unaonyesha kwamba soko zuri liliopo la Utalii kati ya Marekani na Tanzania linafaa kutumiwa vyema kwa kuweka mazingira yatakayostawisha pande zote mbili.
Amesema yapo Makampuni kadhaa ambayo tayari yameshaonyesha nia ya kutaka kuitumia fursa hii ya uwekezaji katika Sekta ya Utalii baada ya kutembelea na kuona maeneo mbali mbali Bara na Zanzibar.
Nao kwa upande wao Mabalozi hao wa Heshima wa Tanzania Bw. Ahmed Issa Alqassim wa San Francisco na Bw. Kjell Berg wa  Minessota wameahidi kutekeleza vyema majukumu yao waliokabidhiwa na Taifa.
Mabalozi hao wameishauri Serikali na Jamii kuhakikisha ule Utalii wa Kiutamaduni { Culture Tourism } ulioanzishwa na Vizazi vilivyopita unafaa kulindwa na kuenziwa.
Wamesema Utalii huu ambao zaidi umejikita katika eneo la Kivazi cha asili umekuwa maarufu  na kufikia hatua ya kuigwa na watu maarufu katika sehemu mbali mbali Duniani.
Wakati wa usiku Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alijumuika pamoja na Wafanyabiashara Waandamizi waliounda kundi la VIP Safari kutoka Nchini Marekani katika chakula cha Usiku.
Tafrija hiyo iliyoshirikisha pia Baadhi ya Mawaziri pamoja na Watendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar ilifanyika katika Hoteli ya Serena Inn iliyopo Shangani Mjini Zanzibar.


No comments:

Post a Comment