Rais wa Mtandao wa TPN Bw. Phares Magesa.
Wazalendo,
Kutokana na tangazo letu ndani ya mtandao wetu la juma lililopita tulipokea majina saba ya wanataaluma walioomba kupendekezwa na TPN kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Jakaya M. Kikwete ili awafikirie kuwateua katika tume ya Katiba inayotarajiwa kuundwa muda mfupi ujao.
Vigezo vilivyotumika katika kupendekeza majina haya ni :
1. Uzoefu wa muombaji katika masuala ya mbali mbali ya kijamii
2. Elimu ya muombaji
3. Jinsia ya muombaji ili kuwe na mchanganyiko
4. Uwakilishi wa makundi ya kitaaluma
5. Uwakilishi wa makundi ya kijamii ndani ya wanataaluma
Majina yanayotakiwa kupendekezwa sio zaidi ya matatu, hivyo basi baada ya kupitia taarifa binafsi (CV/Biodata) za wanataaluma 7 walioomba , kamati ya utendaji ya TPN imependekeza majina yafuatayo yapelekwe ofisi ya Rais wa JMT :
1. Prof. Tolly Salvator Augustin Mbwette, Ph.D (Civil) , Vice Chancellor – Open University of Tanzania
2. Dr. Yahya Abdallah Ipuge, MD, M.Med., Head of Health Promotion Unit- Ifakara Health Institute
3. Bi. Modesta Lilian Mahiga, LLB (Hons), Group Managing Director – Professional Approach Group
Hivyo, basi majina tajwa hapo juu ndio yatawakilisha jumuiya hii ya wanataaluma wa Tanzania, endapo watapata bahati ya kuteuliwa na Mhe. Rais Kikwete basi wahakikishe wanatoa mchango wao katika tume hii ya katiba na hatimae kutupatia katiba nzuri itayokadumu kwa miaka mingine mingi ijayo.
Kwa naiba ya TPN nawashukuru wote walioleta maombi ya kuomba kupendekezwa katika tume hii na nawaomba tuendelee kushirikiana ili hatimae tujenge Tanzania iliyo bora zaidi.
Nawatakia wote kila heri.
Phares Magesa
Rais- TPN.
No comments:
Post a Comment