Wednesday, February 15, 2012

WALIOFUTIWA MATOKEO KURUDIA BAADA YA MIAKA MITATU


Na Fatma A Mzee Habari Maelezo 15/2/2012
Katibu mtendaji wa baraza la Taifa la mitihani Tanzania (NECTA), Dkt Joyce L. Ndalichako ameeleza kuwa jumla ya wanafuzi 3303 wamefutiwa mitihani yao kutokana na kuthibitika kufanya udanganyifu.
DK. Joyce liyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Bwawani mjini zanzibar.
Aliongeza kuwa kati ya hao kuna baadhi ya watahiniwa wameandika matusi katika karatasi zao kamitihani na wengine kuwacha maswali na kutokujibu kabisa maswali ya majibu hayo. Hata hivyo Dkt Joyce alishindwa kujibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari kutokana na kutokufanya majumuisho yote ya mitihani hiyo iliyofanyika nchini.
Aidha alieleza kuwa suwala hilo la udanganyifu linafanyika katika makundi yote matatu ambao ni walimu wazazi pamoja na wanafunzi wenyewe.
Dkt Jooyce ameongeza kuwa waliofutiwa mitihani kulitokana na kikao cha 86 nambari 6 B kilichofanyika tarehe 7-2-2012. Kanuni za baraza la mitihani zinazoeleza kuwa watahiniwa hao hawataruhusiwa kufanya mitihani kwa muda wa miaka mitatu.
Hata hivyo amesema kuwa baraza limewaonea huruma kwa kuwapa hukumu hiyo kwani katika kanuni za NECTA wanafunzi wanaofutiwa mitihani hawaruhusiwi kufanya mitihani tena.
Pia katibu mtendaji huyo aliwataka wasimamizi kuwa makini katika kazi zao na kusimamia kwa uwangali mitihani kwani udanganyifu huwa unamadhara makubwa katika taifa ambapo kutazalishwa wataalamu wasio na viwango hasa katika kipindi hiki ambapo tunaingia katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Wakati huo huo chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimewasimamisha wanafunzi watatu wa chuo hicho baada ya kubainika walitumia vyeti vya kughushi wakati walipojiunga na chuo hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari katika chuo hicho, Vuga mjini Zanzibar, mwanasheria wa SUZA Mtaibu Abdalla Othman amewataja wanafunzi hao kuwa ni Mahfoudhat Hassan Khamis anaesoma digrii ya sanaa, Shafii Suleiman Mringo anaesoma cheti cha teknolojia ya habari na Yussuf Khamis anaesoma cheti cha sayansi ya komputa.

No comments:

Post a Comment