Wednesday, February 15, 2012

MISS TANZANIA 2012 KUZINDULIWA LEO

Shindano la Urembo la Miss Tanzania kwa Msimu wa mwaka 2012 linataraji kuzinduliwa leo jijini Dar es Salaam. 

Kwa Mujibu wa Kampuni ya Lino Intentional Agency, waandaaji wa Shindano hilo,  Uzinduzi huo rasmi unataraji kufanyika katika Ukumbi wa Savanah Longe katikati ya jiji na kuhudhuriwa na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali ambapo pia mdhamini wa mwaka huu wa shindano hilo atajulikana. 

Taji la Miss Tanzania hadi sasa linashikiliwa na Mlimbwende Salha Izrael ambaye alilitwaa katika shindano la Mwaka 2011 na kujinyakulia zawadi ya gari la Kifahari aina ya Jeep. 

Aidha usiku wa leo kutaangushwa bonge la Part kwaajili ya uzinduzi huo. 
Blogu Hii kama dawa kama kawa itakushushia matukio hayo yote moja kwa moja kutoka eneo la tukio.

No comments:

Post a Comment