Tuesday, February 21, 2012

SUGU NA RUGE SASA MAMBO SHWAAAAAAARI.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi  akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na kumalizika kwa mgogoro wa miaka miwili uliotokana na sababu za kimuziki baina ya  Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Katikati) na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba (kulia). Wapatanishi wa mgogoro huo ni  Waziri Dk. Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu.
Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba (kulia) akimsikiliza Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na  mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao uliotokana na sababu za kimuziki uliodumu kwa muda wa miaka miwili. Wapatanishi wa mgogoro huo ni  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu.
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam juu ya  mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao uliodumu  kwa muda wa miaka miwili. Wapatanishi wa mgogoro huo ni  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu. (Picha na Anna Nkinda-Maelezo).
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba  wakipeana mikono leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni ishara ya kupatana na kumaliza kwa  tofauti zao zilizotokana na sababu za kimuziki zilizodumu kwa muda wa miaka miwili. Huku wapatanisha wa mgogoro huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu (kulia) wakishuhudia.

No comments:

Post a Comment