Mkazi wa Kurasini jijini Dar es Salaam Anna Issangya (30) Pichani amepotea kwa muda wa mwezi mmoja sasa katika mazingira ya kutatanisha eneo la Mbagala, mara baada ya kupandwa na malaria kichwani na kutupa vitu vyake vyote alivyovishika.
Akizungumza na MO BLOG kaka wa Anna Simon Issagya amesema dada yake huyo awali alikuwa hana matatizo yeyote ya kusumbuliwa na akili, isipokuwa alipatawa na malaria ghafla na kuanza kutumia dawa huku akiomba Mungu amsaidie kwa kuwa yeye ni mlokole, lakini siku hiyo aliaga nyumbani na kwenda kazini kwake eneo la ZAKIEM – Mbagala bila ya kurudi nyumbani ndipo ndugu zake walipopatwa na wasiwasi.
Amesema walipoona kimya kimezidi siku ya pili walienda kufuatilia kazini na wakaambiwa kwamba dada yao ameondoka, ameelekea mtaani kuhubiri injili, walipotafuta mtaani katika eneo la Nzasa na Majimatitu wananchi wanaoishi maeneo hayo wakasema kuwa wamemuona mtu kama huyo akitupa vitu vyake na kuanza kukimbiakimbia mtaani, na baadhi ya wananchi wakachukua vitu vile wakavipeleka kituo cha Polisi cha Majimatitu Mbagala.
Issangya amesema wameenda kuripoti katika vituo vya Polisi vya Nzansa na Majimatitu Mbagala hivyo wanaomba mtu yeyote akakaye muona mtu huyo katika maeneo hayo atoe ripoti kituo cha polisi kiklichopo karibu naye.
No comments:
Post a Comment