Saturday, February 18, 2012

LEO NI LEO KATIKA SOKA: YANGA NA SIMBA KUITOA TANZANIA KIMASOMASO..??

Timu za Simba na Yanga za Tanzania leo zinaingia dimbani kuvaana na timu za Rwanda na Misri katika michuano tofauti ya kimataifa.
Wakati klabu ya Simba inayoongoza ligi ya Tanzania ikiikabili timu ya Kiyovu ya Rwanda katika uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali leo, watani wao wa jadi Yanga Africans watamenyana na klabu ya Zamalek kutoka Misri katika mechi itakayopigwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga inashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika wakati Simba inawakilisha katika michuano ya Kombe la Shirikisho.
Katika michuano hiyo miwili mikubwa iwapo Simba itafanikiwa kuvuka hatua za kwanza na kuingia katika hatua za makundi inauhakika wa kunyakuliwa zaidi ya shilingi milioni 200 na iwapo Yanga wanaoishikilia nafasi ya pili katika ligi ya nyumba watafanikiwa kushinda mechi sita za kwanza na kuingia katika hatua ya makundi itakuwa na uhakika wa kuzoa zaodi ya shilingi milioni 600.
Mechi zote mbili ya Kigali, Rwanda na Dare s Salaam, Tanzania zinachezwa leo Jumamosi.

No comments:

Post a Comment