Monday, February 20, 2012

KIDUM, LINEX, KHADIJA KOPA, SIKINDE NA ‘KINA RIHANNA’ WAKOLEZA MOTO DAR LIVE.

Walivyowatoa udenda mashabiki.
Msanii akionyesha ukali wake.
Shabiki akilimaindi jukwaa alipopewa fursa ya kuonyesha machejo.
Msanii mdogo mwenye ‘swagger’ za kiutu uzima,  Hamisi Fadhili aka ‘Dogo Lila’, akiimba kwa mbwembwe.









Sehemu ya umati uliofurika kituoni hapo.
Moto mkali uliendelea kuwaka kituo cha maraha cha Dar Live huko Mbagala jijini Dar usiku wa kuamkia leo ambapo wasanii mbalimbali wa Bongo: Linex, Khadija Kopa, Alex Machejo, na makundi ya ngoma za asili ya Machozi na  Mawazo Group, bendi ‘Sikinde Ngoma ya Ukae’,  Dogo Lila  na msanii Kidum kutoka nchini Burundi, wote hao walikamua sambamba na washiriki wa shindano la ‘Vaa, Imba na Cheza,Kama Rihanna’ na kuufanya umati mkubwa ulifoka hapo kupata burudani isiyopimika katika hali yoyote.
Wasanii hao walitumbuiza kwenye Family Day Bonanza ambalo hufanyika kila siku ya Jumapili chini ya usimamizi wa uongozi wa kituo hicho cha Dar Live kilichopo Mbagala-Zakheem jijini Dar es Salaam
Habari/Picha: Musa Mateja/GPL

No comments:

Post a Comment