Saturday, February 18, 2012

JK AONGOZA MATEMBEZI YA HISANI KUSAIDIA UJENZI WA HOSPITALI YA KINAMAMA YA CCBRT JIJINI DAR.

Rais Kikwete akiongoza matembezi ya Hisani kuchangia ujenzi wa hospitali ya kinamama ya Baobab iliyo chini ya CCBRT jijini Dar es salaam. Katika picha kutoka kulia Meya wa Ilala Mh. Jerry Silaa, Meya wa Kinondoni Mh. Mwenda, Bw. Erwin Telemans Mkurugenzi mtendaji wa CCBRT, Rene Meza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya CCBRT Bw. Wilbroad Slaa na kulia kwa Rais ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hadji Mponda na Mkurugenzi wa Vodafone Foundation Bw. Andrew Dunnet pamoja na Mwamvita Makamba wa Vodacom Tanzania katika matembezi hayo leo asubuhi.
Rais Jakaya Kikwete akishiriki katika mazoezi ya viungo kabla ya kuongoza matembezi ya hisani kuchangia   ujenzi wa hospitali ya kinamama matatizo mbalimbali ya uzazi katika hospitali ya CCBRT leo asubuhi jijini Dar es salaam. Matembezi hayo yameanzia katika hoteli ya Golden Tulip na kumalizika katika Hospitali ya CCBRT Mikocheni, matembezi hayo yameandaliwa kwa pamoja na kampuni ya Vodacom Tanzania, Vodafone pamoja na hospitali ya CCBRT Kampeni hiyo inaitwa Find your Moyo.(Picha na IKULU).

No comments:

Post a Comment