Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Arusha ambaye pia ni kocha wa riadha wa timu ya mkoa wa Arusha, John Bayo (kushoto) akizungumza jambo na wanariadha wanaouwakilisha mkoa wa Arusha katika Mashindano ya mwaka huu ya Kilimanjaro Marathon yatakayofanyika kesho mjini Moshi. Kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya CFAO Motors, Alfred Minja walioidhamini timu hiyo kushiriki mashindano hayo. (Picha na Mpigapicha wetu).
Meneja Masoko wa Kampuni ya CFAO Motors, Alfred Minja walioidhamini timu ya Riadha ya Mkoa wa Arusha katika Mbio za Kilimanjaro Marathon 2012, akiwa katika picha ya pamoja na makocha wanaoinoa timu ya mkoa wa Arusha.
Meneja Masoko wa Kampuni ya CFAO Motors, Alfred Minja walioidhamini timu ya Riadha ya Mkoa wa Arusha katika Mbio za Kilimanjaro Marathon 2012, akiwapa mkono wa heri na kuwatakia ushindi wanariadha hao 18, wanaouwakilisha mkoa wa Arusha katika mbio hizo zitakazofanyika kesho mjini Moshi, mkoani Kilimnajaro. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Arusha ambaye pia ni kocha wa riadha wa timu hiyo, John Bayo.
Na.Mroki Mroki,Moshi
Timu ya riadha kutoka Mkoa wa Arusha, imejigamba kuibuka na ushindi mnono katika Mshindano ya mwaka huu ya mbiuo za nyika yajulikanayo kama Kilimanjaro Marathon 2012 yatakayofanyika kesho mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Timu hiyo ambayo, imedhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors ya jijini Dar es Salaam imesema mwaka huu haipo tayari kuachia medali za dhahabu, Shaba na fedha ziende nchini Kenya na badala yake watahakikisha kuwa zinabaki hapa nchini.
“Tumejipanga vizuri sana mwaka huu na wachezaji wetu wote waliingia kambini kujifua vizuri chini ya udhamini mzuri wa CFAO Motors, hivyo watanzania wake tayari kushangilia ushindi”,alisema Kocha wa timu hiyo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Arusha,John Bayo.
Aidha Bayo alisema timu ya Arusha inaundwa na wachezaji mashuhuri na walio na rekodi nzuri za mashindano hayo nay ale ya kimataifa.
Aliwataja wachezaji wanounda timu hiyo ya Arusha iliyo na wakimbiaji 18 kuwa ni Fabiola William, Banuuelia Katesigwa, Flora Kagali, Rebeca Kavina, Daudi Joseph, Mashaka Masumbo, Yohana Masuka na Josepha Elias ambao hukimbia Full Marathon.
Wengine watakao kimbia Nusu marathon (21km) ni Mary Naali, Fabian Joseph, Faustine Mussa, Ezekiel Jafari, Uwezo Lukinga, Rogart John, Joseph Francis, Restituta Joseph, Jacquline Sakilu na Damian Chopa.
Nae Meneja Masoko wa Kampuni ya CFAO iliyodhamini timu hiyo ya mkoa wa Arusha, Alfred Minja, amesema kampuni yake imetumia Shilingi milioni 35 katika mashiondano ya mwaka huu ikiwa ni pamoja na kudhamini timu hiyo na uratimu waa mashindano.
Minja alisema mwaka wa 10 sasa CFAO Motors inadhamini mashindano ya Kilimanjaro Marathon na mwaka 4 sasa kudhamini timu ambazo zimekuwa zikifanya vizuri.
Aidha amesema CFAO Motors itakuwa na meza maalum ya kugawa maji, soda, vitafunwa na burudani ya muziki kwa katika eneo la Mweka ambapo wakimbiaji watakuwa wakigeuzia.
Minja amesema CFAO Motors, mbali na kudhamini wachezaji hao wa timu ya Arusha 18 lakini pia inawakimbiaji wengine 25 wa nusu marathon kutoka jijini Dar es Salaam.
Mashindano ya Mwaka huu ya Kilimanjaro Marathon yanataraji kuwa na shamra shamra za aina yake Ambato pia yatakiwa yanatimiza mwaka wa kumi tangu kuanza kufanyika.
No comments:
Post a Comment