Wednesday, February 22, 2012

WITO KWA WADAU WA SEKTA YA MASWALA YA HARUSI.

Maonyesho ya biashara ya harusi sasa  ni maonyesho makubwa ya harusi nchini yanayojumuisha wadau mbalimbali katika sekta ya harusi kutoka sehemu mbalimbali nchini  Tanzania kwa kuonyesha bidhaa zao na huduma kwa umma kwa ujumla.
“Ndoa ni moja kati ya nyakati za muhimu katika maisha ya binaadamu na sherehe za harusi ni moja kati ya nyakati chache  zinazoleta  marafiki, familia na jamii kwa ujumla  wote kuwa pamoja. Hivyo bila ya msaada kutoka kwa wadau wa sekta ya mambo ya harusi  utambuzi wa kuwa na ndoto ya Harusi bora haiwi yakinifu. Najivunia  katika kutimiza ndoto kugeuka katika ukweli ”.  Alisema mwanzilishi wa Harusi Trade Fair Mustafa Hassanali.
Katika mwaka wake wa tatu sasa, Maonyesho ya Biashara ya Harusi yatakuwa na mambo makuu matatu ,ambayo ni  maonyesho yenyewe, majadiliano na maonyesho ya mavazi. Maonyesho yote yatakusanya zaidi ya wafanyamaonyesho 50 ambao watakuwa wakionyesha bidhaa zao na huduma, kwenye Majadiliano kutakua na wageni kadhaa ambao watakua ni wasemaji  katika uwanja wao wa utaalamu , na kuzungumzia mambo yonayohitajika na yasioitajika  na mambo yote yanayohusu harusi, Maonyesho ya mwaka ya Harusi yatahusisha zaidi ya wabunifu kumi wa mitindo na wamiliki wa maduka ya bidhaa za Harusi ,ambapo bidhaa zao hizo zitaonyeshwa na kuuzwa katika maonyesho ya mavazi ya Harusi ambayo yatafanyika tarehe 31 Machi- 2012 kuanzia saa 2 Usiku nakuendelea.

“Mwaka jana tulikua na wageni  zaidi ya 1500 ambao walihudhuria maonyesho haya, tunatarajia wageni zaidi mwaka huu . Kuvuna faida za matumizi na sehemu pana na masoko ya karibu zaidi, tunawaomba wachuuzi wote wa mambo ya  harusi kuchukua fursa hii ya kila mwaka ya kuonyesha katika maonyesho haya ya  kipekee ya harusi nchini “Alisema Meneja wa Masoko wa Harusi Trade Fair  Hamis K Omary .
Hadi sasa zaidi ya washiriki  18 wa maonyesho ya Harusi  tayari wamedhibitisha kushirki,miongni mwao ni  EndePa event planners, Mkoma Bay lodge iliyopo Pangani, kearsleys travel, Binti Afrika, Wedding Bells, Rose fashion designs, Blind Tiger, MH Gallery, Dia’s , Green Chef na cocktails, GRM production, Pure Beauty , Lotus Creative concepts ,kwa kutaja chache tu.

Harusi Trade Fair 2012 itafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee kwa siku 3 mfululizo kuanzia tarehe 30 marchi- 1 Aprili  kuanzia saa 4:00 asubuhi nakuendelea.
“ Tukiwa tunamalengo makubwa sana ya kutangaza  Harusi Trade Fair na kuitangaza Tanzania kama  mahali  pa Harusi na kama sehemu ya kupumzikia kwa maharusi duniani, ningependa kuwashukuru washirika wetu wote kwa kutuunga mkono kwa miaka yote iliyopita na kuendelea kuomba mashirika na kampuni mbalimbali kutuunga mkono kwa kudhamini Harusi Trade Fair 2012’’ . Alimalizia Afisa Mahusiano, Amisa Juma
Harusi Trade Fair 2012 imedhaminiwa na  Clouds Media group, Global Outdoor Systems. H.Models and 361 Degrees

No comments:

Post a Comment