Wednesday, February 22, 2012

WAZIRI NAGU AKUTANA NA UJUMBE WA WAWAKILISHI WA UCHUMI NA BIASHARA KUTOKA CHINA.

aziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji  Dk.Mary Nagu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Uchumi na Biashara wa watu wa Jamhuri ya China nchini Tanzania walipomtembelea leo ofisini kwake  jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Lin Zhiyong ambaye ni Mwalikishi mpya na kulia  ni Zhao Zhongqiu ambaye amemaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini.(Picha na Anna Nkinda – Maelezo).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji  Dk. Mary Nagu akisalimiana na Mwakilishi Mkuu mpya wa Uchumi na Biashara wa watu wa Jamhuri ya China nchini Tanzania Lin Zhiyong leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam . Zhiyong anachukua nafasi ya Zhao Zhongqiu ambaye amemaliza  muda wake wa kufanya kazi hapa nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji  Dk. Mary Nagu akiongea jambo na aliyekuwa Mwakilishi Mkuu wa Uchumi na Biashara wa watu wa Jamhuri ya China nchini Tanzania Zhao Zhongqiu leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam . Zhongqiu alimtembelea waziri huyo kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji  Dk.Mary Nagu akiongea na ujumbe wa wawakilishi wa Uchumi na Biashara wa watu wa Jamhuri ya China nchini Tanzania walipomtembelea leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam . Ujumbe huo uliongelea mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na jinsi ya kuimarisha mahusiano ya kiuchumi na kibiashara kati ya Tanzania na China.

No comments:

Post a Comment