Thursday, February 23, 2012

WAZIRI MKUU PINDA ZIARANI SHINYANGA.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na  Afisa Biashara wa  Wilaya ya Bariadi, Leonard   Batigashaga akiwa katika ziara ya mkoa wa Shinyanga Februari 22, 2012. Kulia ni Mkewe Mama Tunu Pinda.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimana na Wananchi wa  na viongozi wa wilaya ya Meatu baada ya kuwasili katika kijiji cha Mwandoya akiwa katika ziara ya Mkoa wa Shinyanga Februari 22, 2012.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,  Ally Nasoro Rufunga na  wapili kushotoni  Mkuu wa Wilaya ya Meatu Abihudi Saideya.
Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina ipo katika hatari ya kuvunjwa kwa vile imejengwa kwenye eneo la akiba la barabara. Pichani Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akionyeshwa  na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Nasoro Rufungaalama inayoonyesha  sehemu ya ukuta wa ofisi hiyo unatakiwa kuvunjwa. Nyumba hiyo imejengwa kwenye kijiji cha Mwandoya wilayani Meatu.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

No comments:

Post a Comment