Wednesday, February 22, 2012

NBC YAJITOSHA KUDHAMINI GOFU LA WANAWAKE

 Meneja Udhamini na Matukio wa NBC, Bi. Rachel Remona Kimambo ( wa pili kushoto)  akikabidhi mfani wa hundi ya shs milioni kwa Nahodha wa Kitengo cha gofu ya Wanawake cha Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam, Vivienne Mwaulambo kusaidia mashindano yao yanayotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo katika klabu hiyo ijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni maofisa wa NBC na viongozi wa kitengo hicho cha gofu.
 Nahodha wa Kitengo cha Gofu ya Wanawake cha Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam, Vivienne Mwaulambo (kushoto) akizungumza kabla ya kupokea msaada  msaada huo kutoka benki ya NBC. Katikati ni Meneja Udhamini na Matukio wa NBC, Bi. Rachel Remona Kimambo na kulia ni Katibu wa kitengo, Joyce Svarva.
 Maofisa wa NBC pamoja na wa Kitengo cha Gofu ya Wanawake cha Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam wakipiga picha ya pamoja katika hafla hiyo jijini Dar es  salaam leo.
Nahodha wa Kitengo cha Gofu ya Wanawake cha Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam, Vivienne Mwaulambo (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya maofisa wa NBC baada ya kupokea msaada msaada huo kutoka benki ya NBC. Kutoka kushoto ni,  Arden Kitomari, Meneja Chapa na Matangazo, Eddie Mhina; Mshauri wa  awasiliano na Meneja Udhamini na Matukio wa NBC, Bi. Rachel Remona Kimambo.

No comments:

Post a Comment