Tuesday, February 14, 2012

NBC YA NUNUNA HISA ASILIMIA 10.87 KWENYE KAMPUNI YA MIKOPO YA NYUMBA, TMRC

Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NBC Bw. Lawrence (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi bilioni moja kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Mortgage Refinance Company Limited (TMRC) Bw Rished Bade katika hafla iliyofanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo leo.
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) leo imekabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi bilioni moja kwa Kampuni mahususi ya Kutafuta Fedha na Kutoa Mikopo ya Muda Mrefu ya Nyumba iitwayo Tanzania Mortgage Refinance Corporation (TMRC) ikiwa ni kiasi cha kununua hisa za asilimia 10.87 kwenye kampuni hiyo. TMRC ni taasisi ya kifedha inayomilikiwa na mabenki mbali mbali kwa lengo la kusaidia mabenki yaweze kutoa mikopo ya muda mrefu ya nyumba kwa wateja.
Lengo kuu la TMRC ni kusaidia kutoa fedha kwenye soko la kifedha la Tanzania kwa ufanisi, na kuzilenga fedha hizo kwa mabenki wanachama kwa viwango vya ushindani. Hii itawezesha upatikanaji wa makazi kwa watanzania, na pia kuchangia maendeleo ya masoko ya mitaji.
Shughuli hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki ya NBC, ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bwana Lawrence Mafuru.
Akizungumza kwenye tukio hilo, Bwana Mafuru alisema: “Tunaamini kuwa fedha hizi zitaiaidia TMRC katika juhudi zake za kuwawezesha Watanzania wapate kumiliki makazi bora. Kitendo hiki kinaonyesha dhamira ya NBC katika kusaidia sekta ya mikopo ya nyumba Tanzania ”
Hundi hiyo imepokewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TMRC, Bwana Rished Bade mbele ya viongozi wa ngazi ya juu wa kampuni hiyo pamoja na wawakilishi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Mwezi Oktoba 2011, NBC pamoja na benki nyingine sita zilisaini mkataba na Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) kwa ajili ya kuwawezesha Watanzania kipata makazi bora zaidi.

Washauri wa masuala ya habari NBC kulia ni Redemptus Massanja na Eddie Mhina.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Mortgage Refinance Company Limited (TMRC) Bw Rished Bade kulia akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kukabidhiana hundi ya shilingi bilioni moja kutoka benki ya NBC (katikati)Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NBC Bw. Lawrence Mafuru na kushoto ni Mortgage Finance Specialist kutoka benki kuu Bw. Baraka Munisi.
Maafisa mbalimbali wakiwa katika mkutano huo leo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Mortgage Refinance Company Limited (TMRC) Bw Rished Bade kulia na Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NBC Bw. Lawrence Mafuru waliokaa wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa kutoka NBC, BOT na TMRC.

No comments:

Post a Comment