Tuesday, February 21, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA SHAMBA LA MAHINDI NA NYUKI WA KISASA LA WAZIRI MKUU KIJIJI CHA VILOLO KATAVI.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea shamba la mahindi la Waziri Mkuu Mizengo Pinda, lililopo Kijiji cha Vilolo wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Katavi na Rukwa leo Februari 20, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea shamba ufugaji wa Nyuki wa kisasa la Waziri Mkuu Mizengo Pinda, lililopo Kijiji cha Vilolo wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Katavi na Rukwa, Februari 20, 2012. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR).

No comments:

Post a Comment