Monday, February 27, 2012

JOHNSON MBWAMBO ACHAGULIWA MWENYEKITI MPYA WA JET.

Baadhi ya viongozi wapya wa Chama cha waandisdhi wa habari wa mazingira (JET) Tanzania waliochaguliwa. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti mpya Johnson Mbwambo na wa kwanza kushoto ni katibu mtendaji wa JET John Chikomo. Wa kwanza kulia ni makamu mwenyekiti Aisha Dachi na anayefuata ni katibu mkuu Chrsostom Rweyemamu.
Baadhi ya wanachama wa JET wakishiriki zoezi ya kupiga kura kuchagua viongozi wapya wa chama hicho.
Picha ya pamoja ya viongozi wa JET waliomaliza muda wao Wa tatu kutoka kushoto ni mwenyekiti mstaafu Deodatus Mfugale.
Baadhi ya wanachama wa JET waliohudhuria mkutano mkuu wa chama hicho. (Picha zote na Nathaniel Limu).
Na.Nathaniel Limu
Mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama cha waandishi wa habari wa mazingira Tanzania (JET) umemchagua Johnson Mbwambo kuwa mwenyekiti wake kwa kipinidi cha miaka mitatu ijayo.
Mbwambo ambaye ni mkurugenzi wa bodi ya gazeti la Raia mwema alipata kura 44 za ndiyo na nne zilimkataa.
Mwandishi wa habari mkongwe wa TBC radio Aisha Dachi amechaguliwa kuwa makamu mwenyekiti baada ya kupata kura 47 dhidi ya moja iliyomkataa.
Chrysostom Rweyemamu ametetea vyema nafasi yake ya ukatibu mkuu baada ya kupata kura 46 dhidi ya moja iliyomkataa.
Viongozi wote hao wa ngazi za juu katika chama hicho cha JET hawakuwa na wapinzani kitendo kilichosababisha wapigiwe kura za ndiyo na hapana.
Waliochaguliwa kuunda kamati ya utendaji na kura zao kwenye mabano ni Ali Haji Hamadi (40), Dk. Ellen Otaru (38), Salome Kitomari (31), Judica Losai (31), Zainabu Mwatawala (30) na Gerald Kitabu (27).
Akitoa shukurani zake za dhati kwa wananchama wa JET kwa kumwezesha kushinda nafasi hiyo ya uenyekiti, Mbwambo amesema kipaumbele chake ni kuweka mikakati itakayosaidia chama hicho kusimamakwa miguu yake badala ya kuendelea kutegemea wafadhili tu.

No comments:

Post a Comment