Mbunge wa Bumbuli Mh January Makamba akifafanua jambo ndani ya kipindi cha jahazi la Clouds FM kuhusiana na hoja yake binafsi aliyoitoa hivi karibuni, ya kuliomba Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania liazimie, kwa kauli moja, kuitaka Serikali, katika Mkutano ujao wa Saba wa Bunge, kuleta Muswada wa Sheria ya Kudhibiti Upangaji wa Nyumba za Makazi (Rental Housing Act):
1.Itakayoweka utaratibu na udhibiti wa sekta ya upangaji wa nyumba nchini kwa ujumla,2. Itakayowezesha kuanzishwa kwa Wakala wa Udhibiti wa Sekta ya Nyumba – Real Estate Regulatory Authority (RERA),3.Itakayoainisha wazi haki na wajibu wa wapangaji na wenye nyumba,4.Itakayoweka utaratibu wa haraka na rahisi zaidi kwa wapangaji na wenye nyumba kupata haki zao,5.Itakayodhibiti na kuweka adhabu kwa vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wapangaji,6.Itakayoweka utaratibu wa ukaguzi wa viwango na hali za makazi ya kupanga,7.Itakayozuia na kuweka adhabu kwa utaratibu wa kutoza kodi ya nyumba kwa miezi sita au mwaka mzima.
No comments:
Post a Comment