Sunday, July 8, 2012

CRDB BANK YAPIGA JEKI UANZISHWAJI WA CHUO KIKUU CHA NYANDA ZA JUU KUSINI

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiluthei Dayosisi ya Konde Askofu Dr. Dr.Israel Mwakyolile akipokea hundi za fedha zenye thamani ya shilingi millioni 60 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dr.Charles Kimei zilizotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Nyanda za Juuu ya Kusini katika hafla iliyofanyika jijini Mbeya hivi karibuni.Kushoto ni Askofu Isaya Mengele wa Jimbo la Njombe . Jumla ya Shillingi Millioni 120 zilipatikana katika harambee hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dr.Charles Kimei akikabidhi picha yake kwa Ndugu Boimanda aliyenunua kwa Shillingi Millioni mbili katika harambee ya kuchangia fedha kwa  ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Nyanda za Juuu ya Kusini katika hafla iliyofanyika jijini Mbeya hivi karibuni. JUMLA YA SHILLINGI MILLIONI 120 zilipatikana amabapo benk ya CRDB ilichangia shillingi millioni 65. Kushoto ni  Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiluthei Dayosisi ya Konde Askofu Dr. Dr.Israel Mwakyolile na kulia ni Askofu Isaya Mengele wa Jimbo la Njombe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dr.Charles Kimei akivishwa heshima ya uchifu wa mikoa ya nyanda za juu kusini na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheri jimbo la Njombe Askofu Isaya Mengele baaada ya kuongoza harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Nyanda za Juu ya Kusini katika hafla iliyofanyika jijini Mbeya hivi karibuni. JUMLA YA SHILLINGI MILIONI 120 zilipatikana ambapo benk ya CRDB ilichangia shillingi millioni 65.Kushoto ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiluthei Dayosisi ya Konde Askofu Dr. Dr.Israel Mwakyolile.
Viongozi nchini wametakiwa kutenda haki, uzalendo na kuacha ubinafsi kwa jamii ili kutokomeza ufisadi unalitikisa taifa la Tanzania.
Aidha, wametakiwa kuwa mfano wa miongoni mwa viongozi wachache wenye uchungu na uzalendo kwa nchi, akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei kwa kumudu kuongoza taasisi kubwa ya kifedha pamoja na kutoa ajira kwa mamia ya wazalendo.
Kauli hiyo ilitolewa na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Dayosisi ya Kusini Njombe, Isaya Mengele wakati akiongoza ibada ya harambee ya kuchangia Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini kinachotarajiwa kuanzishwa Kanda ya  mwishoni mwa wiki iliyopita.
Alisema viongozi wengi wakiwemo mawarizi na wabunge wamekuwa wakipigiwa kelele za ufisadi na wananchi waliowapa dhamana na kwamba wameshindwa kuwa wazalendo, kuwafanya wananchi kukosa imani nao.
“Japo hawajathibitishwa lakini kelele za wananchi kuhusu viongozi kugubikwa na ubinafsi na kukosa uzalendo wa nchi yao limekuwa likiongezeka kila wakati… lakini tuna baadhi ya viongozi wachache wenye uadilifu ambao wana uchungu na uzalendo na nchi yao kwa kutoa ajira za mamia ya watanzania akiwemo Dk. Kimei,”alisema.
Aliongeza kuwa “Mtu anapoitwa fisadi hata kama hakuna ushahidi ina maana anakuwa anakwenda kinyume na maadili yaliyo mema…kwa miaka mingi Dk. Kimei amekuwa akiongoza taasisi hiyo ya kifedha hapa nchini lakini haijawahi kutokea kukutwa na kashfa yoyote na imekuwa miongoni mwa taasisi zinazotoa mchango mkubwa kwa nyanja zote za jamii” alisema Askofu Mengele.
Alisema mchango wa benki ya CRDB ni mkubwa kwa jamii nzima hata kanisa linatambua na kwamba inastahili kupata nishani ya heshima chini ya usimamizi wa Dk. Kimei.
Akizungumzia kuhusu kumtolea mungu, alisema moyo wa kumtolea mungu ni kibali kilichotolewa kwa kila mtu na kwamba haina maana kuwa matajiri peke yao ndiyo wenye mamlaka bali kila mtu ana jukumu la kutoa kile alichonacho na kitahesabiwa.
Akifungua Harambee hiyo, Dk. Kimei alisema benki yake imepata changamoto ya kuchangia jamii ikiwemo chuo hicho kitarajiwa kutokana na wadau wakubwa wa benki yake ni watanzania wote bila kujali itikadi.
Alisema kitakapoanzishwa chuo hicho kitasaidiwa kupunguza gharama, mlundikano wanafunzi kwenye vyuo vingine pamoja na umbali kupata huduma hiyo.
“Vyuo hivi ni muhimu kuanzishwa kwenye kanda hii kwa sababu itasaidia kuondoa mlundikano kwenye vyuo vingine, kupunguza gharama kwa walezi na wazazi wa kanda hii kutokana na hali ngumu ya maisha kwa sasa pia kukaa karibu na familia vijana wengi watasoma kwa usalama zaidi, nidhamu itaongezeka na kuwaepusha na vitendo visivyofaa” alisema.
Akifafanua zaidi Dk. Kimei alisema kuwepo kwa vyuo vikuu kunachangia maendeleo katika jamii husika kutokana na kuongezeka kwa huduma mbalimbali ikiwemo za kibisahara na za kibenki.
“Benki yangu inachangia Sh. milioni 50 na itashirikiana na bega kwa bega katika maendeleo ya ujenzi wa chuo hiki kikuu kitarajiwa” alisema Dk. Kimei.
Naye  Mkuu wa Chuo Cha Ualimu Makumila, Mchungaji Dk. Gwamaka Mwankenja alisema mpango mkakati wa ujenzi na uanzishwaji wa chuo hicho zinahitajika Sh. bilioni 33.6 ili kukamilisha mradi huo.
Alisema katika kipindi cha mwaka 2012/2013 zinahitajika kukusanywa Sh. bilioni 2 ambapo hadi sasa wamefanikiwa kukusanya michango mbalimbali kutoka kwa washarika na wadau Sh. 209,231,870.
Katika harambee hiyo, Dk. Kimei alifanikiwa kukusanya Sh. milioni 120 kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwemo zilizotolewa na benki yake.

HABARI NA MO-BLOG


No comments:

Post a Comment